Ep 2-TERRE PROMISE OU ENFER

GrandsLacsTV - Podcast
GrandsLacsTV - Podcast
Ep 2-TERRE PROMISE OU ENFER
Loading
/

TERRE PROMISE OU ENFER

Ni kipindi kinacho letwa kwenu namuungano inayo itwa Initiative Chrétienne pour la Paix, la Réconciliation et le Développement – ICPRD, Kipindi hiki kina lenga ku himiza wakahaji kuhusu uwongozi bora, Amani pia uchimbaji madini halali nalenyi kuheshimu aki zabinadamu mutaani Mwenga.

Advertisement

Je, tunawezaje kuchimba madini ilioko ardhini bila kuharibu maisha ya watu, mazingira, na mshikamano wa jamii?
Je, tunawezaje kuchimba madini bila kukiuka haki za binadamu?

Kipindi hiki kitajibu nakuingilia kwa kina hali gani madini inachimbwa wilayani Mwenga, katika jimbo la Sud-Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini lakini pia lenye mvutano kutokana na uchimbaji madini haramu unayo fanyika na shirika ambazo haziheshimu sheria  inchini inayo husu uchimbaji.

Mtazamo wetu pia utakuwa juu ya mradi unaotekelezwa na ICPRD: plaidoyer pour la bonne gouvernance des ressources naturelles dans lebterritoire de Mwenga, mradi unaolenga kuhimiza uchimbaji madini halali, kuheshimu sheria na mazingira, ukikazia zaidi mazungumzo kati ya wachimbaji, wakaaji wa Mwenga na mamlaka za serikali ya Congo.

Tunayo imani ya kwamba utetezi na haki yabinadamu, kulenga utawala bora ama bonne gouvernance katika uchimbaji madini Mwenga siyo tu kuweka mukazo kwa uchimbaji madini halali na unaolinda mazingira, bali pia nikuzuia nakupiganisha migogoro na kuimarisha mshikamano wa kijamii kati ya watu wote wanao husika.

 

Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Advertisement